App yetu inakuruhusu kukamilisha aina tofauti za oda. Endapo unataka kusafirisha watu au mizigo, utahitaji chombo cha usafiri. Tunazo kazi kwa watu wenye ujuzi wa kutengeneza nyumba, wabebaji wa mizigo kwa miguu, na wataalamu wengine. Jisajili haraka, pakua app, na uangalie oda zinazopatikana kwenye huduma ulizochagua.
App yetu inaonesha maelezo yote ya oda, pamoja na bei yake na njia ya malipo. Watumiaji wengi huchagua malipo yasiyo ya fedha taslimu, ambayo ni rahisi kwa wote, watoa huduma na wateja.
Kiasi cha kamisheni utakacholipa kinategemeana na eneo, promosheni za sasa na masharti ya ushirikiano wetu. Unaweza kufanya kazi kila wakati kwa kiwango cha chini cha asilimia. Kila wakati app yetu inakuonesha ni kiasi gani utakachokipata kwa kukamilisha oda.